Kuja umpige mwenyewe

Ukiwa katika mgogoro na mtu alafu mtu aliye kando akuambie mpige mwambie "kuja umpige mwenyewe".

Sasa banaeeh Asubuhi twavuka ferry sasa tushashuka wajua pale ferry watu wakiwa wengi kuna msongamano wa watu ma tuktuk na magari sasa kuna huyu bwana aliye bebwa kwa pikipiki akaona jamaa wa tuktuk ameziba njia akaanza kujibizana na yeye kalameni wengi hapo nyuma wakamshawishi "mpige mjinga huyo" ndugu akaona ana sapoti ya watu akamsukuma jamaa wa tuktuk akadhani ndivyo kesi imeisha hivyo kumbe jamaa alingoja asongeshwe mbele kwa vile alikuwa mlangoni mwa tuktuk hapo akaeka park katika tuktuk akamfuata mbio kama mshale kabla jamaa hajashuka katika piki piki jamaa wa tuktuk alishampiga madondi si haba wale makalameni waliomwambia apigane walikuwa mashabiki sasa daaah! mambo gani haya sasa huyu jamaa aliangusha simu katika pilka pilka sijui kama alirudishiwa ingelikuwa mimi ningerudi nyumbani nilale

Posted Jun 25, 2026, 6:43 AM UTC

147
Loading comments…