Nimepeleka dem kwa family gathering

Last weekend kulikuwa na family gathering ya extended family huku Eldoret, nikasema ndio opportunity ya kuintroduce dem yangu officially. Nilikuwa nimejiambia hii ni mara ya kwanza family wengi watamuona, so nilikuwa na confidence kila kitu itaenda poa.

Tulifika, nikaanza kumtambulisha kwa kila mtu. Mathe alimpenda immediately, shosho akambariki, aunties wakaanza kumuuliza kama anajua kupika mursik na traditional vegetables. Nilikuwa nashangaa vile ameshaingia kwa family haraka hivyo.

Baadaye tukatoka nje kidogo kupiga story na cousins. Ndipo mmoja wa uncle zangu akapita, akamtazama vizuri halafu akasema, "Wewe si nakujua?"

Dem yangu akacheka akasema, "Inawezekana."

Hapo ndipo movie ilianza.

Uncle akasema alikuwa anamjua kupitia church ya zamani. Before conversation iishe, neighbour wetu wa zamani akafika akasema walikuwa wanaishi estate moja Pioneer. Dakika chache baadaye cousin yangu mwingine akasema walikuwa wanaenda tuition pamoja. Ata wife wa uncle akaingia kwa conversation akasema waliwahi kufanya biashara pamoja miaka kadhaa iliyopita.

Mimi nilikuwa nimesimama hapo nikijiuliza mbona kila mtu ana history na huyu msichana, na mimi ndio nimemleta.

Tulipokuwa tunaenda nyumbani nilimuuliza, "Mbona kila mtu Eldoret anakujua?"

Akacheka tu akasema, "Si nilikulia hapa."

Hapo ndipo nilirealize kitu moja. Watu husema Eldoret imekua sana, lakini ukiishi hapa enough years, utaona hii town ni village yenye imevaa town. Kila mtu anaonekana kuwa na connection na kila mtu.

Ama ni family yangu tu ndio wanajua watu wote? 😂

Posted Jun 27, 2026, 8:02 PM UTC

11
Loading comments…